
ROBINSON KELVIN
.....Here you will be close to all news around the World of social, political and economical ones...
Friday, 10 October 2014
Friday, 3 October 2014
Sunday, 27 July 2014
ORODHA KAMILI YA WASHINDI WA TUZO ZA AFRIMMA 2014 DIAMOND NA LADY JAYD WAKIWEMO

Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)
Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)
Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)
Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)
Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)
Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)
Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)
Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)
Best African Group 2014- P-square (Nigeria)
Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)
Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)
Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)
Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)
Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)
Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)
Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)
Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)
Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)
Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)
Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)
Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)
Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)
Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)
Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)
Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia
Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka
Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio
HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA DIAMOND PLATNUMZ...NI MWENDO WA VIPARAAAA...!!
Sunday, 20 July 2014
JK AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME SONGEA VIJIJINI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amezindua mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa
Umeme Vijijini (REA) utakaowanufaisha wakazi wa Mkoa wa Ruvuma
utakaochangia kuongeza kasi ya maendeleo vijijini.
Rais
Jakaya Kikwete yuko katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya
maendeleo katika mkoa huo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya
kuwa kila mwananchi anapata huduma ya nishati ya umeme.

Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
amewahakikishia wakazi hao kwamba hadi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu
vijiji vyote vilivyoko katika mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya
II watakuwa tayari wanatumia nishati hiyo kwa wale watakao wamemudu
gharama ya Shilingi Elfu Ishirini na Saba ya kuunganishiwa nishati
hiyo.
Imeelezwa
kwamba mradi wa usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Ruvuma
utagharimu kiasi cha Tsh. 26.53 bilioni zitakazohusisha ujenzi wa njia
za umeme zenye msongo wa kilovolti 33 zenye jumla ya urefu wa km 538,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti 11 yenye urefu wa km 23,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa km 272,
ufungaji wa transfoma 129 za ukubwa mbalimbali pamoja na kuunganisha
wateja 7,488.

Mradi
huu utatekelezwa na kampuni ya Lanka Transfomers Limited, (LTL) ya
nchini SRILANKA kwa mkoa wa Ruvuma. Mradi huo unatarajiwa kukamilika
ifikapo Juni 2015 na kunufaisha wakazi wa wilaya za Songea, Tunduru,
Mbinga na Nyasa.
Pamoja
na uwepo wa mradi huo pia kuna mradi wa kuongeza nguvu ya umeme kwenye
wilaya za Mbinga na Tunduru unaotekelezwa na kampuni ya Taikai Co.Ltd
ambapo tayari amekamilisha survey ya vituo vyote na ameshawasilisha
transifoma ya kituo cha Tunduru. Prof. MUHONGO amesema mradi wa kuongeza
nguvu ya umeme utagharimu kiasi cha pesa za kitanzania Shilingi bilioni
2.27 zitakazohusisha ujenzi wa vituo viwili vya kuongeza nguvu ya umeme
kutoka kilovoti 11 hadi kufikia kilovoti 33 kwa ajili ya kufikisha
umeme katika vijiji vilivyoko mbali.
Vituo
hivyo vitakuwa na transifoma zenye uwezo wa kilowati 3,000 (3.0MW) kila
kimoja. Kwa upande wake Mbunge wa MBAMBABAY Captain JOHN KOMBA
ameishukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza ilani
ya uchaguzi ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya
barabara hasa madaraja, kuwawekea umeme, na kupandishwa hadhi kituo cha
afya na kuwa hospitali ya wilaya.
Miradi
ya REA awamu ya II imeanza kutekelezwa rasmi Novemba 2013 na inatakiwa
kukamilika ifikapo Juni2015 kwa nchi nzima hivyo kuchangia katika
kuongeza kiasi cha wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme kufikia
asilimia 30.
Meneja
wa Shirika la umeme nchini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi,
Bi Salome Nkondola akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi ya
umeme kwa mkoa wa Ruvuma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete
Rais
Jakaya M. Kikwete akichukua mkasi kwa ajili ya kukata utepe tayari
kuelekea katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme
wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, kulia kwake ni Waziri mwenye dhamana na
nishati Prof. Sospeter Muhongo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa
serikali wakiwepo Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi, Waziri
wa Nishati na Madini, Waziri wa Ujenzi wakiwa wameshika utepe tayari
kwa Rais kuukata na kuelekea kubonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya
uzinduzi wa mradi huo wa umeme.
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akibonyeza kitufe
Rais akifurahia uzinduzi mara baada ya zoezi hilo kukamilika

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akielekea eneo la jukwaa mara baada ya kuwasili
katika eneo palipofanyika uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijijini
unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wilaya ya Nyasa mwishoni
mwa wiki, kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter
Muhongo.








Burudani wakati wa sherehe hizo
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)