
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.

Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali.
Kiliendelea kudai kwamba, sangoma h




Baada ya mke wa Huruka kuokolewa kufanyiwa ukenge, mwanamke mwingine wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma huyo.
Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publisher ambayo ilifika eneo hilo usiku baada ya kutonywa na chanzo chake, Tabu alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia gesti hiyo.
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo.
Baada ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo, Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo.
Katika
hali ya kushangaza mke wa Tabu alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka
kumpiga mganga wake ambaye alikuwa akitaka kummalizia matatizo huku
wanawake wengine wakiwaomba radhi waume zao na kudai walirubuniwa.
Akizungumizia
mkasa huo mke wa Tabu alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani
ambapo alimwita majina yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo
akaanza kumtajia matatizo yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia
mama huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli
ndipo alianza kumuamini.
MWISHO WA SAKATA
Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake.
Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua.

MWISHO WA SAKATA
Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake.
Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua.
No comments:
Post a Comment